Archive for June 2016

Mlipuko wakumba hoteli mjini Mogadish

Mlipuko mkubwa umekumba hoteli moja katikati ya mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kuna sauti za ufyatulianaji wa risasi katika kile kinachoaminika huenda ni shambulio la wapiganaji wa al-Shabab.
Kulingana na mwandishi wa BBC Ibrahim Aden mjini Mogadishu, mlipuko huo ulikumba hoteli ya Naso Hablod ikiwa ni hatua chache kutoka kwa uwanja wa ndegewa mji huo.
Hakuna ripoti zozote za majeruhi.
Ripoti zinasema kuwa huenda kulikuwa na mlipuko wa pili.
Wapiganaji wa al-Shabab hutekeleza mashambulio ya mara kwa mara katika mji huo kwa lengo la kuiangusha serikali inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.
''Walianza na mlipuaji wa kujitolea muhanga na baadaye kuvamia.Kwa sasa wako ndani na ufyatuliaji mkubwa wa risasi unaendelea'' ,alisema msemaji wa polisi meja Nur Farah.

SWITZERLAND YASONGA MBELE EURO2016 KWA KUICHAPA POLAND 5-4.

 
Jakub Blaszczykowski aliiweka mbele Switzerland kabla ya Xherdan Shaqiri kusawazisha kupitia bao zuri.
Image copyrighMchezaji huyo wa Stoke alimfunga Lukas fabianski kupitia shambulio la 'Bycycle kick' kwa lugha ya Kiingereza.
Image copyright
Mchezaji aliyesajiliwa hivi majuzi na klabu ya Arsenla Granit Xhaka alikosa penalti kwa upande wa Switzerland baada ya mechi hiyo kuisha na sare ya 1-1
Poland itakutana na Croatia ama Portugal katika robo fainali ya michuano ya Euro2016 baada ya kuishinda Switzerland kwa Penalti.

SIMU BANDIA ZA UZAUZWA CONGO NA MSUMBIJI.


Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la Mwananchi, yenye kichwa cha habari ‘simu bandia zapata soko Msumbiji, Congo’.

Gazeti hilo limeripoti kuwa Siku mbili baada ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima simu feki, wafanyabiashara wa simu hizo wamepata soko jipya katika nchi za Msumbiji na Congo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hilo, baadhi ya vijana waliokutwa wakizunguka madukani kuzikusanya, walisema wanazinunua na kuzisafirisha kwenda huko kwa ajili ya kuziuza kwa watumiaji. Walisema katika nchi hizo kuna soko kwa sababu zinakamata mawasiliano kama kawaida.

Gazeti hilo limemnukuu Lawrence Kyondo ambapo amesema wanazinunua kwa bei ya makubaliano na kwenda kuziuza katika soko la nje……….>>>’hatujaanza hii biashara leo, siku nyingi isipokuwa wenye maduka walikuwa bado wagumu kuziuza wakidhani hazitazimwa

POLISI JIJINI MWANZA WAPAMBANA NA MAJAMBAZI KWA MASAA 16



Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi,wameuawa katika majibizano ya risasi na askari polisi mkoani Mwanza,alfajiri ya kuamkia jana jumapili katika mapango ya mlima wa Utemini yaliyopo kata ya Mkolani jijini Mwanza.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi,amewataja majambazi waliouwa katika majibizano ya risasi usiku kucha kuwa ni Omar Francis Kitaleti mkazi wa Nyegezi Kona,said Khamis Mbuli maarufu kama fundi bomba mkazi wa bugarika na jambazi mwingine ambaye jina lake bado halijafahamika.

Amesema majambazi hayo yalikuwa yamejificha kwenye mapango ya mlima wa Utemini kabla ya askari polisi kufanikiwa kuyaua.

Jambazi mmoja aliyeuawa ambaye hajafahamika jina lake mwenye umri kati ya miaka 20 hadi 25 alikuwa akiwashambulia polisi kwa kutumia bastola ambapo baada ya polisi kumpiga risasi walimpekua na kumkuta akiwa na bastola aina ya Chinese,iliyokuwa na risasi tatu ndani ya magazine,huku majambazi wengine waliokuwepo kwenye mapango hayo wakiendelea kujibishana kwa risasi na askari polisi.

Kamanda Msangi ameongeza kwamba Ijumaa Juni 3,askari polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama,walimkamata Omar Francis Kitaleti kwa jina maarufu kiberiti,mkazi wa Nyegezi Kijiweni ambaye alikuwa akituhumiwa kuhusika katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwenye maduka ya M-pesa,Tigo Pesa na Airtel money jijini Mwanza ambaye baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika katika matukio hayo na aliwataja wenzake anaoshirikiana nao na mahali walipojificha.

Amesema ilipotimu majira ya saa kumi na moja kamili jioni siku ya Jumamosi Juni 4,polisi walifika katika mlima huo na walipoyakaribia mapango hayo ghafla walianza kushambuliwa kwa risasi na majambazi waliokuwa wamejificha ndani ya mapango hayo.

Katika mapambano hayo ya risasi na askari polisi,risasi hizo ziliweza kumpata jambazi mwenzao aitwaye Omary Francis Kitaleti aliyekuwa anawaongoza askari polisi na kufariki dunia papo hapo, na risasi nyingine ilimjeruhi askari kwenye unyayo wa mguu wake wa kulia.

Amesema polisi kwa kutumia mbinu za medani za kivita waliweza kuzingira maeneo hayo ya mlima wa utemini hadi alfajiri ya kuamkia Jumapili Juni 5,huku wakijibishana risasi na majambazi hao na baada ya kuona yamezidiwa nguvu huku kukikaribia kupambazuka ndipo yalipoamua kuondoka ndani ya mapango hayo kwa kurusha bomu moja la kutupa kwa mkono huku yakizidisha mapigo ya risasi kwa kutumia silaha walizokuwa nazo.

Ameongeza kuwa polisi wamekamata bunduki moja aina ya SMG iliyokuwa na risasi nane na kisu kimoja.

Kamanda Msangi amesema majambazi watatu walifanikiwa kutoroka kutoka kwenye mapango hayo kuelekea maeneo ya Nyasaka na baada ya jambazi mmoja kubaini kuwa askari polisi walikua wanamfuatilia alitoa bunduki  na kutaka kuwapiga askari polisi lakini polisi waliweza kumuwahi na kumfyatulia risasi sehemu mbalimbali za mwili wake na kufariki dunia papo hapo.

Amesema askari polisi wamefanya upekuzi kwenye mapango ya mlima wa Utemini na kufanikiwa kupata vitu mbalimbali vilivyoachwa na majambazi hao ambavyo ni pamoja na risasi nne,kisu kimoja chenye damu,kofia ya kuficha uso nyeusi moja (mask),jiko la stove,masufuria ya kupikia, unga wa mahindi,sukari,dagaa,chakula kilichopikwa,ngoma mbalimbali,na simu tatu za mkononi.

Askari aliyejeruhiwa amelazwa hospitali ya rufaa ya bugando na hali yake inaendelea vizuri,polisi bado wanaendelea na msako wa kuwatafuta majambazi waliofanikiwa kutoroka.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo alitembelea kwenye mapango ya Utemini na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu

Jamie Vardy anatarajiwa kutia saini Arsenal.

Kijana wa miaka 29 Jamie Vardy kutoka Leicister City anatarajiwa hii leo kutoa majibu iwapo atajiunga na Club ya Arsenal.
Mchezaji huyo anatarajiwa kutoa majibu kama atajiunga na Arsenal kabla hajaelekea kwenye michuano ya Euro ya mwaka huu akiwa na timu ya taifa ya Uingereza.
Arsenal tayari wamefikia makubaliano na Leicester na wamemwekea mezani Vardy kitita cha fedha kwa miaka minne.
Vardy bado alikuwa anatafakari kama awaache Mbweha kuelekea kwa washika Bunduki. Itakumbukwa Vardy aliisaidia sana Leicister katika kutwaa taji la Ligi kuu akifunga mabao 24

MUHAMMED ALI KUZIKWA IJUMAA.

Mwili wa aliyekuwa bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali, umewasili mjini Louisville, Kentucky, ambako atazikwa siku ya Ijumaa.
Mwili wa bondia huyo wa zamani ulisafirishwa kwa msafara wa magari kutoka uwanja wa ndege wa Louisville.
Mazishi yake yanatarajiwa kuwa hafla kubwa ya umma.
Ali alikuwa mmoja wa wanamichezo maarufu zaidi duniani katika karne hii ya 20

- Copyright © FURAHA MEDIA - Blogger Templates - Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -