Kizza Besigye ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa Rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi wa nchi hiyo uliofanyika hivi karibuni.
Inaonekana leo itakuwa ni nafasi nzuri kwa upande mashtaka kurekebisha makosa katika hati za mashtaka dhidi ya Kizza Besigye ambapo itakuwa mara ya pili kufikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma hizo za uhaini kwani awali alifikishwa mahakani kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa iliyopita katika mji huo wa Moroto .
Besigye alishikiliwa na polisi kwa muda wa siku mbili ambapo alifikishwa mahakamani huku shughuli za mahakama zikiwa zimekisha.
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafuasi wake ambao wamekuwa wakisema hakuruhusiwa kuwasiliana na wanasheria wake.
Besigye anakabiliwa na tuhuma za kujitangaza kuwa mshindi wa rais wa Uganda mwezi February japo mshindi aliyetangazwa na mahakama ya juu nchini Uganda ni Rais Yoweri Museveni ambaye aliapishwa wiki iliyopita kuwa Rais wa Uganda.