Posted by : FURAHA MEDIA Wednesday, July 6, 2016

Madaktari nchini India wamepandikiza pua mpya katika uso wa mvulana wa miaka 12 iliokuwa imemea katika paa lake la uso.
Pua ya Arun Patel iliharibika alipougua ugonjwa wa homa ya kichomi ambapi maambukizi hayo yaliharibu pua yake akiwa mtoto mdogo.
Wazazi wa Arun walimchukua na kumpeleka katika daktari mwengine katika kijiji cha jimbo la kati la Madhya Pradesh ambapo aliugua kichomi mda mfupi baada ya kuzaliwa.
Miaka kadhaa baadaye,kundi moja la madaktari katika mji wa Indore liliamua kufanya upasuaji usiokuwa wa kawaida ambapo Arun alipata pua mpya.
Upandikizaji kama huo ulifanywa nchini China mwaka 2013 ambapo mtu mmoja ambaye  pua yake iliharibika katika ajali alipewa pua mpya.

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © FURAHA MEDIA - Blogger Templates - Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -