Posted by : FURAHA MEDIA Wednesday, July 6, 2016

Ureno imekuwa nchi ya kwanza kuingia fainali ya michuano ya Euro 2016 baada ya kuzima ndoto za Wales kwa kuichapa magoli 2 - 0 katika mechi ya nusu fainali mjini Lyon nchini Ufaransa.
Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo ameendelea kuwa mwiba kwa wapinzani kwenye mashindano hayo baada ya kupachika goli kabla mshambuliaji wa zamani Manchester United Luis Nani kupigilia msumari wa moto kwenye kidonda kwa kupachika goli la pili.
magoli yalitupiwa dakika ya C Ronaldo (50), na Nani (53)
Kwa matokeo hayo Ureno sasa itakutana na mwenyeji Ufaransa au Ujerumani katika mechi ya fainali.

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © FURAHA MEDIA - Blogger Templates - Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -