Archive for July 2016

Nuh Mziwanda Asema Hawezi Kuingilia Bifu la Shilole na Video Queen wa Video ya ‘Jike Shupa.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo chini ya label ya ‘LFLG’, ameiambia Clouds FM kuwa kwa sasa hawezi kuingilia ugomvi usiyomuhusu.
“Wale ni wanawake kwa hiyo zile ni tofauti zao, siwezi kuingilia na siwezi kuongea chochote, yule demu mimi nilimlipa pesa yake ya video akafanya, kazi yangu kamaliza masuala yake yanayoendelea kimpango wake,” alisema Nuh.

Aliongeza, “Kwa hiyo siwezi kuingilia na wala sitaki kufuatilia na wala sitaki kujua kwa sababu nimeshamalizana nae. Yale ni maisha yake binafsi siwezi kuingilia,”
Shilole na video queen wa video ya ‘Jike Shupa’ wamekuwa wakitupia vijembe katika mitandao ya kijamii.

URENO YATINGA FAINALI EURO 2016.

Ureno imekuwa nchi ya kwanza kuingia fainali ya michuano ya Euro 2016 baada ya kuzima ndoto za Wales kwa kuichapa magoli 2 - 0 katika mechi ya nusu fainali mjini Lyon nchini Ufaransa.
Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo ameendelea kuwa mwiba kwa wapinzani kwenye mashindano hayo baada ya kupachika goli kabla mshambuliaji wa zamani Manchester United Luis Nani kupigilia msumari wa moto kwenye kidonda kwa kupachika goli la pili.
magoli yalitupiwa dakika ya C Ronaldo (50), na Nani (53)
Kwa matokeo hayo Ureno sasa itakutana na mwenyeji Ufaransa au Ujerumani katika mechi ya fainali.

MTOTO APANDIKIZWA PUA INDIA.

Madaktari nchini India wamepandikiza pua mpya katika uso wa mvulana wa miaka 12 iliokuwa imemea katika paa lake la uso.
Pua ya Arun Patel iliharibika alipougua ugonjwa wa homa ya kichomi ambapi maambukizi hayo yaliharibu pua yake akiwa mtoto mdogo.
Wazazi wa Arun walimchukua na kumpeleka katika daktari mwengine katika kijiji cha jimbo la kati la Madhya Pradesh ambapo aliugua kichomi mda mfupi baada ya kuzaliwa.
Miaka kadhaa baadaye,kundi moja la madaktari katika mji wa Indore liliamua kufanya upasuaji usiokuwa wa kawaida ambapo Arun alipata pua mpya.
Upandikizaji kama huo ulifanywa nchini China mwaka 2013 ambapo mtu mmoja ambaye  pua yake iliharibika katika ajali alipewa pua mpya.

Diamond Aweka Sanamu za Mafuvu ya Watu Ofisini Kwake, Je ni Ishara ya ‘Kifreemasons’????.


Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times).

Lakini miaka ya hiki karibuni kumekuwa na imani kwa watu kuwa freemasons ni imani ya kishetani ambayo imekuwa ikitumiwa na mastaa wakubwa duniani ili kufanikiwa zaidi kipesa na kuwa mashabiki wengi.

Hakuna aliyewai kuthitisha kwamba ni freemasons kama baadhi ya mitandao inavyoripoti, lakini wadau mbalimbali wa mambo duniani wamekuwa wakitoa na kuonyesha alama mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu hao ili kutambuana.

Hata hivyo Diamonda ameonekana katika picha mbalimbali akipost kwenye nitandao ya kijamii Diamond huku akiwa amenaonyesha alama za Freemasons pia hivi karibuni alipost picha akiwa ofisini kwake huku pembeni kukiwa na sanamu za fuvu za watu

Diamond Platnumz Jumanne hii alipost video instagram akiwaeleza mashabiki wake kuhusu kuchelewa kwa kazi yake mpya ambayo ilikuwa itoke wiki iliyopita, lakini ndani ya video hiyo ambayo inaonyesha kuchukuliwa ofisini kwake, imeonyesha sanamu za mavufu mawili ya watu na kuibua maswahi mengi kwa mashabiki huwenda zikawa alama za kifremasons ambazo zimekuwa zikitumika na mastaa mbalimbali waliofanikiwa duniani...

- Copyright © FURAHA MEDIA - Blogger Templates - Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -