Archive for February 2017
HISTORA YA NDEGE AINA TAI
Hujambo msomaji wa makala ya jicho letu karibu katika mwendelezo wa makala ndege aina mbalimbali na leo tunaangazia ndege aina ya tai .endelea kusoma makala hii adhimu.
Tai ni ndege kama walivyo ndege wengine, ingawaje wao
wana sifa za pekee hasa kutokana na ufundi wao wa kuwinda, kupaa na uwezo wao
mkubwa wa kuona mbali.
Kwa sababu kuna aina mbalimbali, hata maumbile yao
yanatofautiana. Aina ya tai mwenye uzito mkubwa kabisa ni aina ya “Steller’s sea Eagle” ana uzito unaofikia kilogramu 6.7
Tai
mwenye mabawa marefu kuliko wote ni aina ya “White Tailed Eagle” mabawa yake yana jumla ya urefu wa sentimita
218.5, sawa na mita 2.185.
Tai aina ya “Phillipine
Eagle” ndio wanaoongoza kwa urefu, wao wanafikia sentimita 100.
tai ana sifa mbalimbali kama ilivyo kwa ndege wengine japo ndege huyu ameonekana kuwa na sifa tofauti na ndge wengine ulimwenguni.
Tai hupaa juu sana angani wala shomoro na kunguru
hawawezi kufika huko. Hakuna ndege yeyote mwenye uwezo wa kupaa juu sana
kufikia kimo anachofikia tai, labda awe tai mwenyewe.
Mara nyingi huwa tunawaona
mwewe wakipita sehemu fulani, shomoro na kunguru huwazomea, lakini tai hataki
vurugu hizo.
Unatakiwa kuwa na maono na uyatazame
maono yako bila kuangalia pembeni mpaka uyapate au uyatimize hiyo ndiyo siri ya
kuelekea mafanikio yako, haijalishi vikwazo unavyokumbana navyo njiani, wewe
kaza mwendo bila kurudi nyuma. bila kurudi nyuma.
tai wana uwezo mkubwa na wana uwezo Wa kuona kitu
kilichoko umbali wa kilometa tano.
Tai akiona mawindo yake huangalia pale
pale na huanza kwenda kukamata mawindo
hayo kwa kasi kubwa.
Haijalishi kama kuna vipingamizi vyovyote njiani, tai
hatabadili kuangalia mawindo yake hadi akamate mawindo.
Tai hali mizoga. Anakula kile tu alichokamata yeye.
Tunajifunza nini? Kuwa makini na kile unacholisha macho
yako, masikio yako hasa kuangalia filamu na luninga. Usipende kutumia mizoga (mambo machafu) kwa sababu utaiharibu
nafsi yako na maisha yako hayatakwenda kwa kasi kubwa ya mafanikio..