Michuano ya kombe la FA nchini England iliendelea tena Jumatano kwa mchezo mmoja ambapo West ham United walikuwa wakichuana na Manchester United.
Matokeo ya mchezo huo Manchester waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 kupitia kwa Marcus Rashford na Marouane Fellaini dk ya 67 kipindi cha pili , Huku bao la west ham likifungwa na James Tomkins dk ya 79 kipindi cha pili, na Manchester United watakutana na Everton hatua ya nusu Fainali katika uwnaja wa Wembley.
Katika mwendelezo wa ligi kuu ya England Everton wametosha na nguvu na Crystal palace ukiwa ni mchezo pekee uliopigwa hapo jana.
Klabu ya soka ya Barcelona Jumatano ilivuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Atletico Madrid huku Mabao yote ya Altletico Madrid yakifungwa na Antoine Griez-mann na bao la pili likifungwa kwa mara nyingine na Antoine kwa njia ya penalti .
Kwa matokeo hayo Atletico Madrid wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 3 -2 baada ya awali kufungwa 2-1 na Barcelona katika Uwanja wa Camp Nou.
Katika mchezo mwingine Bayern Munich imefakiwa kutinga nusu fainali baada ya kuitoa Benfica kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa jana .
Mabao ya Benfica yamefungwa na Raul Alonso Rodriguez na Anderson Souza Conceicao , na magoli ya Bayern Munich yakifungwa na Arturo Vidal na Thomas Muller .
Hivyo Atletico Madrid na Bayern Munich zinaungana na Real Madrid ya Hispania pamoja na Manchester City katika nusu fainali ambayo droo yake itapangwa siku ya Ijumaa.
Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Magonjwa Marekani (CDC) kimethibitisha kwamba virusi vya Zika husababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo na ubongo kudumaa.
Kumekuwa na mjadala mkubwa na suitafahamu kuhusu uhusiano kati ya virusi hivyo na watoto kuzaliwa na vichwa vidogo tangu kuongezeka kwa visa vya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo Brazil.
Mkurugenzi mkuu wa CDC Tom Frieden amesema hakuna shaka kwamba virusi vya Zika vinasababisha watoto kuzalwia na vichwa vidogo, tatizo ambalo kwa Kiingereza hujulikana kama microcephaly.
Maafisa wa CDC wamesema kwamba bado wanawashauri wanawake wajawazito kutozuru maeneo ya Amerika Kusini na visiwa vya Caribbean, ambako maambukizi ya virusi hivyo yameripotiwa.
Virusi vya Zika huenezwa sana na mbu ingawa kumeripotiwa pia visa vya watu kuambukizwa virusi hivyo kupitia kufanya mapenzi.
Kumeripotiwa visa 346 vya maambukizi ya virusi hivyo Marekani.
Jumatatu, maafisa nchini humo walionya kwamba mlipuko wa sasa wa virusi vya Zika huenda ukaathiri sana Marekani na wakaomba kutolewe ufadhili zaidi.
"Kila kitu tunachofahamu kuhusu virusi hivi kinaonekana kuwa cha kuogofya zaidi ya tulivyodhania," alisema Dkt Anne Schuchat kutoka CDC.
Virusi vya Zika viligunduliwa mara ya kwanza mwaka 1947 nchini Uganda, lakini dalili za kuambukizwa virusi hivyo hazijakuwa kali. Wengi wa wanaoambukizwa walikuwa wakipatwa na homa ambayo si kali sana, mwasho na maumivu katika maungio.
Mlipuko wa sasa ulianza mwishoni mwa mwaka 2015 nchini Brazil na dalili zake zimekuwa kali.
Watoto karibu 200 wamefariki kutokana na virusi hivyo.
Kanda ya video iliyotumwa kwa maafisa wa serikali ya Nigeria kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Boko Haram inaonesha baadhi ya wasichana waliotekwa eneo la Chibok wako hai.
Ni miaka miwili tangu kutekwa kwa wasichana 276 kutoka shule moja katika mji wa Chibok.
Ni wasichana 15 wanaoonekana kwenye kanda hiyo ya video ambayo inaaminika ilipigwa Siku ya Krismasi.
Video hiyo imepeperushwa hewani na shirika la utangazaji la marekani la CNN.
Maafisa wa Nigeria wamesema mashauriano kati ya serikali na wapiganaji hao wa Kiislamu yanaendelea lakini yatasalia kuwa siri kwa sababu za kiusalama na ili kuzuia wanaofanikisha wazungumzo hayo wasitambulike.
Mwandishi wa BBC aliyeko Abuja anasema video hiyo imewapa matumaini baadhi ya raia wa Nigeria kwa sababu inaonesha baadhi ya wasichana wako hai.
Lakini baadhi wanasema hali kwamba ni wasichana wachache sana waliooneshwa kwenye video hiyo inaibua wasiwasi kuhusu hatima ya wasichana hao wengine walioonekana kwenye video hiyo.
Kanda hiyo ya video ndiyo ya kwanza kutolewa ikiwaonesha wasichana hao tangu mwezi Mei mwaka 2014.
Serikali ya Nigeria imekosolewa kwa kushindwa kuwakomboa wasichana hao.
Kwa muda mrefu, kitambulisha mada #BringBackOurGirls (Turejeshee wasichana wetu) kilivuma sana mtandao wa Twitter.
Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama ni mmoja wa watu mashuhuri walioshiriki katika kampeni ya kupigania kukombolewa kwa wasichana hao.
WAKAZI wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake wamempongeza Rais John Magufuli kwa hatua aliyochukua ya kuahirisha maadhimisho ya siku ya Muungano na kuokoa zaidi ya Sh bilioni mbili na kuagiza fedha hizo zitumike kufanya upanuzi wa Barabara ya Ghana kuelekea Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Pamoja na pongezi hizo, wamemuomba Rais Magufuli baada ya barabara hiyo kukamilika kufanyiwa upanuzi, ipewe jina la “Barabara ya Muungano” kama njia ya kuienzi kauli yake hiyo aliyoitoa kwa wakazi wa jiji hilo.
Rais Magufuli akiwa Chato mkoani Geita kwa ajili ya mapumziko, juzi alitangaza kuahirisha maadhimisho ya siku ya Muungano mwaka huu na kuagiza fedha ambazo zingetumika kwa vinywaji, halaiki, gwaride na vyakula ambazo ni zaidi ya Sh bilioni mbili, zitumike kufanya upanuzi wa Barabara ya Ghana – Airport.
Kadhalika alielekeza siku hiyo iwe siku ya mapumziko ya kawaida kwa Watanzania kuiadhimisha wakiwa katika shughuli zao binafsi
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limezindua kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Songosongo wilayani Kilwa mkoa wa Lindi chenye uwezo wa kupokea futi za ujazo milioni 70 kwa siku kutoka kwenye visima na kwa kuanzia kitapokea futi za ujazo milioni moja.
Kwa sasa wanafanya majaribio hadi kufikia Juni 30, mwaka huu futi zote za ujazo milioni 70 zitakuwa zimeungana na gesi inayotoka Mnazi Bay katika eneo la Somangafungu na kuanza kusafirishwa kwa bomba la gesi kwenda jijini Dar es Salaam.
Akizindua mtambo huo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk James Mataragio, alisema kufikia Juni 30, mwaka huu bomba la gesi litasafirisha gesi ya futi za ujazo bilioni 10.27 kwenda jijini Dar es Salaam.
Dk Mataragio alisema mitambo ya Songosongo ina uwezo wa kuchakata futi za ujazo milioni 140 katoka visima vinne na Kisima cha Kiliwani -North kitatoa gesi futi za ujazo milioni 20 hadi 30 kwa siku.
“Kwa kuwa mitambo yetu bado ni mipya kitaalamu hatuwezi kuingiza gesi nyingi kwa wakati mmoja, hivyo gesi huingizwa katika mitambo kidogo kidogo kupima uwezo wake lakini mpaka mwezi Juni gesi yote itakuwa imefika jijini Dar es Salaam kwa kutumia bomba la gesi,” alisema Dk Mataragio.
Alisema majaribio yanafanyika ili kupima uwezo wa mitambo kuhimili kiwango cha gesi inayoingia na kuichakata katika viwango vinavyotakiwa na ujazaji wa gesi kwenye bomba na kupima mgandamizo wa gesi.
Pia kuisukuma kwenda Somangafungu ambapo itakutana na ile inayotoka Madimba na kisha kuweka katika mgandamizo sawa na kusafirishwa hadi Dar es Salaam.
Dk Mataragio alisema mitambo hiyo ya kuchakata gesi ya Songosongo inayomilikiwa na serikali kwa asilimia 100, kwa sasa itakuwa ikipokea gesi kutoka katika vitalu viwili ambavyo ni Kiliwani inayomilikiwa na Ndovu Resources na Songosongo inayomilikiwa na Pan African Energy Tanzanie-PAET.
Timu za Barcelona na Bayern Munich zimeanza vizuri michezo yao ya kwanza ya hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Ulaya.
Barcelona, wakicheza katika uwanja wao wa Camp Nou, wamechomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid, mshambuliaji Luis Suarez akifunga mabao yote mawili.
Na bao la Atletico Madrid likifungwa na Fernando Torres ambae pia alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi mbili za njano.
Nao Bayern Munich wakiwa wenyeji wa Benfica wameshinda kwa bao 1-0 kwa bao lilowekwa kambani na kiungo Arturo Vidal.
Ongezeko la idadi ya watu wanaonyongwa ulimwenguni lilisababisha watu zaidi kuuawa kwa njia hiyo mwaka uliopita ikilinganishwa na kipindi chochote tangu mwaka 1989,shirika la haki za kibibaadamu la Amnesty International limesema.
Takriban watu 1634 walinyongwa mwaka 2015,ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Iran,Pakistan na Saudia Arabia walihusika na asilimia 89 ya watu wote walionyongwa duniani.
Image copyrighP
Amnesty International
Image captiJumla hiyo haishirikishi China ambapo Amnesty International imesema kuwa maelfu zaidi waliuawa lakini rekodi zake zikafichwa.
Kwa upande mwengine,kundi hilo limesema kuwa kwa mara ya kwanza mataifa mengi duniani yalifutilia mbali hukumu ya kunyonga.
Mataifa ya Fiji,Madagascar ,Congo Brazaville na Suriname yalibadilisha sheria zao mwaka 2015,huku Mongolia ikipitisha sheria mpya itakayoanza kutekelezwa baadaye mwaka huu.
Image copyright
Vifaa vinavyotumiwa na serikali ya China kuwashinikiza watu kukubali makosa
ImageAmnesty imesema kuwa China bado inaongoza miongoni mwa mataifa yanayonyonga watu.Inakadiriwa kwamba maelfu ya watu walinyongwa huku maelfu ya wengine wakipewa hukumu ya kunyongwa mwaka 2015.