Posted by : FURAHA MEDIA
Wednesday, May 4, 2016
Kampuni ya Apple imepoteza nembo yake ya biashara nchini China, kwa maana kwamba kampuni moja inayouza mikoba na bidhaa nyengine zilizotengezwa na ngozi inaweza kuendelea kutumia ''iPhone''.
Mahama kuu ya Beijing iliamua kwa kuipendelea kampuni ya teknolojia nchini humo Xintong Tiandi,kulingana na gazeti rasmi la serikali nchini humo.
Nembo ya ''IPHONE'' inatumika kuuza bidhaa za ngozi za kampuni ya Xintong Tiandi mwaka 2010.
Apple ilitaka jina hilo kutumika kwa bidhaa zake za kielektroniki mwaka 2002 lakini haikuidhinishwa hadi mwaka 2013.
Xintong Tiandi inauza mikoba,mifuko ya simu pamoja na bidhaa nyengine zilizotengezwa na ngozi zikiwa na jina ''IPHONE'' na herufu ''R'' ya usajili.