Gavana wa jimbo la Alberta nchini Canada ametangaza hali ya hatari wakati moto mkubwa wa msituni unapoteketeza maeneo ya mji wa Fort McMurray.
Maafisa wanasema kuwa nyumba 1600 na majengo mengine yameharibiwa na moto huo ambao sasa unakaribia uwanja wa ndege wa mji huo.
Waziri mkuu nchini Canada amesema kuwa moto huo umesababisha hasara ya kiwango kikubwa.
Watu wa mji wa Fort McMurray ambao ni 80,000 wamehamiswa.
2. Kasich ajitoa mchujo wa chama cha Republican
John Kasich amejitoa kwenye kinyanganyiro cha mchujo wa kugombea urais katika chama cha Republican na kumuacha Donald Trump kama mgombea wa pekee.
Bw Kasich alitoa tangazo hilo kwenye mkutano na waandishi wa habari nyumbani kwake katika jimbo la Ohio.
Hatua hiyo inatoa fursa kubwa kwa Bw Trump kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba.
Trump anasema kuwa ana matumaini ya kuchangisha zaidi ya dola billioni moja kwa kampeni yake.
3. Chama tawala Uturuki kuchagua kiongozi
Ripoti kutoka nchini Uturuki zinasema kuwa chama tawala cha PKK kitakutana baadaye mwezi huu kumchagua kiongozi mpya kufuatia wiki kadha za tofauti kati ya viongozi wawili wakuu wa chama hicho.
Mkuu wa chama waziri mkuu Ahmet Davutoglu hatarajiwi kugombea tena.
Taarifa kuhusu kufanyika kwa mkutano usio wa kawaida ziliibuka baada ya Bw Davutoglu kuelezea kutoridhishwa na sera fulani za rais Recep Tayyip Erdogan, ikiwemo mipamgo yake ya kuifanyia katiba mabadiliko.
4. Maafikiano ya kusitisha vita Syria
Marekani inasema kuwa makubaliano yameafikiwa na Urusi ya kuongeza muda wa usitishwaji mapigano nchini Syria ikiwemo kwenye mji unaokumbwa na mapigano wa Aleppo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry amesema tayari kumekuwa na kupungua kwa ghasia lakini mapigano bado yanaendelea.
Kerry amesema kuwa Marekani na Urusi watafuatilia usitishwaji huo wa ghasia na kupelekwa kwa misaada.
Taarifa za makubaliano hayo ziliungwa mkono na wanachama wa baraza la usalama la umoja ma mataifa wanaokutana mjini New York.
5. Katumbi atangaza atawania urais DR Congo
Mwanasiasa maarufu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba. Mfanyibiashara huyo na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga alitoa tangazo hilo kupitia kwa mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa katiba ya Congo Rais Joseph Kabila anatakiwa kuondoka madarakani mwaka huu lakini wapinzani wake wana hofu kuwa huenda ana mipango ya kusalia madarakani.