Posted by : FURAHA MEDIA
Monday, May 2, 2016
Mcheza tenisi wa Bulgaria Grigor Dimitrov ameomba radhi baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu pale alipoibamiza chini mara tatu fimbo yake ya kuchezea baada ya kukubali kichapo dhidi ya Diego Schwartzman katika michuano ya wazi ya Istanbul.
Mbulgaria huyo aliyekuwa akilisaka taji lake la kwanza katika kipindi cha miaka miwili alipoteza kwa seti 6-7,5-7,7-6, 7-4,na 6-0.
Dimitrov alipewa onyo kali aliporusha kwa mara ya kwanza na kwa hasira fimbo yake ya kuchezea mapema mnamo seti ya tatu na kisha akapewa adhabu kwa kurudia tukio hilo. Huku akiwa nyuma kwa seti 5-0,alifanya tena kosa kama hilo na kumpa mpinzani wake ushindi wa wazi.
''Nimeiangusha familia yangu,Timu yangu,mashabiki wangu kwa tabia mbaya ambayo kwa kweli ninaomba radhi''alisema mchezaji huyo nambari 29 duniani katika mchezo wa tenisi.
Nidhamu ya mchezaji huyo mwenye miaka 24 ilimpatia ushindi na kikombe Schwartzman mwenye miaka 23 katika michuano hiyo aliyoshiriki kwa mara ya kwanza.