Posted by : FURAHA MEDIA Monday, May 2, 2016

Meneja wa Leicester Claudio Ranieri amesema huenda akashindwa kutazama mechi muhimu ya leo jioni kati ya Chelsea na Tottenham.
Iwapo Tottenham watashindwa kuondoka na ushindi uwanjani Stamford Bridge, basi Leicester watatawazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu wa 2015/16.
"Ningependa sana kutazama mechi hiyo ya Tottenham lakini nitakuwa kwenye ndege nikisafiri kutoka Italia,” Ranieri amesema.
"Mamangu anatimiza umri wa miaka 96 na ningependa sana kula naye chakula cha mchana. Nitakuwa mtu wa mwisho Uingereza kufahamu (matokeo).”
Mwitaliano huyo hajawahi kushinda ligi kuu katika maisha yake ya ukufunzi lakini sasa Leicester wanahitaji alama mbili pekee kutawazwa mabingwa baada yao kutoka sare 1-1 na Manchester United Jumapili.
Ranieri hata hivyo amesema anatarajia Spurs, waliosalia na mechi tatu, waongeze muda wao wa kusubiri kushinda taji.
Iwapo Spurs watashinda leo basi Leicester wanaweza kutawazwa mabingwa wakifanikiwa kulaza Everton Jumamosi.
"Akilini mwangu, Tottenham watashinda mechi zao zote tatu," alisema. "Naangazia sana mechi dhidi ya Everton."

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © FURAHA MEDIA - Blogger Templates - Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -