Posted by : FURAHA MEDIA
Saturday, May 28, 2016
Mshirikishe mwenzako
Mapigano makali yametokea Kaskazini mwa Syria wakati kundi la Islamic State linajaribu kutwaa mji unaodhibitiwa na waasi wa Marea.
Islamic State walitekeleza shambulio la asubuhi mapema, wakiwa na makombora, mizinga na magari yaliowekwa bomu.
Kundi hilo limekuwa likikaribia eneo hilo siku za hivi karibuni.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa raia wamejipata katikati mwa mapigano hayo wakijaribu kutoroka.