Awali iliropotiwa kuwa Shule nane kaskazini mwa Afrika Kusini zilichomwa na waandamanaji.
Maandamano nchini Afrika Kusini yana historia ya kubadilika na kuwa ghasia,ikianzia miaka ya nyuma ya utawala wa wakoloni ambapo wakaazi waliokasirika walikuwa wakiharibu mali ya serikali kuonyesha kutopendelea jambo fulani.
Ni zaidi ya miaka 20 sasa tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake na inaonyesha kuwa hatua hiyo haijasahaulika.
Watu hukasirishwa kwa kile wanasema ni hali ya kujikokota kwa serikali kuwapatia huduma kama vile nyumba,umeme na maji na hivyobasi kuamua kufanya uharibifu.
Lakini visa hivyo vimekosolewa na serikali kwa kuwa waandamanaji uharibu vitu muhimu kama vile shule,maktaba na kliniki.
Mwishowe jamii hizo husalia zikihitaji huduma hizo,serikali inasema.