Maelfu ya watu wanatarajiwa
kujitokeza leo mjini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za rumba
Papa Wemba.
Leo ndiyo ni siku ya kwanza ya kipindi cha siku tatu za maombolezo rasmi ya kumuenzi mwanamuziki huyo nchini humo.
Posted by : FURAHA MEDIA
Monday, May 2, 2016
Wemba, 66, aliyesifika kote duniani kama mmoja wa wanamuziki nguli wa nyimbo za rumba kutoka DR Congo, alifariki baada ya kuzirai akitumbuiza mjini Abidjan wiki moja iliyopita.
Mwanamuziki huyo, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, anatarajiwa kuzikwa Jumatano.
Rais Joseph Kabila ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuhudhuria ibada ya wafu leo kwa heshima ya marehemu mjini Kinshasa.