Vilabu tajiri katika ligi kuu ya Uingereza vitatawala kwa miongo miwili ijayo kufuatia ushindi wa klabu ya Leicester kulingana na mkufunzi Claudio Ranieri.
Kikosi cha Leicester kiligharimu pauni milioni 57 ,kikiwa ndio cha bei ya chini zaidi ya timu zilizopo katika nusu ya kwanza ya jedwali la ligi hiyo.
Fedha nyingi hujenga timu kubwa na kama kawaida timu kubwa hushina.Sasa tunaweza kusema ni asilimia 99 ,alisema Ranieri.
Msimu ujao itakuwa hali kama hiyo na miaka 10 ama 20 ijayo,hali itakuwa kama kawaida kwamba timu kubwa ndizo zitakazoshinda,alisema meneja wa Leicester.
Ranieri alisema kwamba ushindi kama wa timu yake hutokea mara moja katika kipindi cha miaka 20 akitoa mfano wa Nottignham Forest mwaka 1978 na Blackburn Rovers 1995.