Posted by : FURAHA MEDIA Saturday, May 28, 2016

Darasa la Mbuga ya Ngorongoro katika chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha(Ajtc) wakishangilia mara baada
ya kuibuka washindi katika michano ya utangazaji iliyofanyika chuoni hapo.

Michuano ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangaza Arusha
 (A.J.T.C) imemalizika hii leo ambapo mshindi wa kwanza hadi wa mwisho amejulikana.

Darasa lililoibuka kidedea katika mashindano hayo yaliyochukua takribani siku tano linatambulika kwa jina la Mbuga ya Ngorongorongoro.

Mashindano hayo aliyohusisha madasa 13, darasa la Ngorongoro limejishindia kombe lenye thamani ya Tsh 10,000 pamoja na pesa taslimu Tsh 150,000.

Nafasi ya pili katika michuano hiyo Utangazaji ilichukuliwa na darasa linaloitwa Mlima Kilimanjaro huku wakijinyakulia tsh10,000 na darasa la Serengeti limeshikili nafsi ya tatu na kupewa zawdi fedha taslimu Tsh 75,000.
 
Mkurugenzi wa chuo hicho cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha bw Joseph Mayagila amewapongeza wanafunzi wote walioshiriki na kuwataka waendelee kujituma katika masomo yao ili wafanye vizuri katika tasnia ya uandishi wa habari na utangazaji.

Akifunga mashindano ya utangazaji katika ukumbi wa chuo hicho mkuu wa wa kitengo cha utangazaji chuo hapo Bw Onesmo Elia Mbise  amewapongeza darasa la Mbuga ya Ngorongoro anakuwataka wanafunzi wote chuo hapo kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya utangazaji ili kujiimarisha na kuwa vizuri katika fani hiyo.

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © FURAHA MEDIA - Blogger Templates - Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -