Posted by : FURAHA MEDIA Wednesday, May 4, 2016



Mgombea wa Republican Ted Cruz amejiondoa kwenye kinyanganyiro cha kugombea urais nchini marekani na kutoa fursa kwa Donald Trump kuwa mgombea mteule wa chama hicho.
Cruz alitoa tangazo hilo muda mfupi baada ya kubainika kuwa alikuwa ameshindwa katika mchujo wa jimbo la Indiana. Aliwaambia wafuasi wake kuwa alikuwa amejitolea zaidi kwa kampeni yake lakini sasa hana njia nyingine ya kuendelea. Akitoa hotuba yake ya ushindi Trump alimtaja Cruz kama mshindani aliye mgumu.

2. Sanders amshinda Clinton mchujo Indiana

SandersImage copyrightAP
Image captionBw Sanders amesema bado anaendelea na kampeni
Katika upande wa chama cha Democratic Bernie Sanders amemshinda kwa kura chache Hillary Clinton. Matokeo hayo haya hivyo hayatathiri uongozi wa Hillary Clintom kwa sababu bado ana nafasi kubwa ya kuwa mgombea mku wa chama hicho

3. Moto mkubwa wazua taharuki Canada

Fort McMurrayImage copyrightCBC
Image captionWakazi wa mji wa Fort McMurray wametakiwa kuhama
Jimbo la Alberta nchini Canada linaendelea na shughuli kubwa zaidi ya kuhamisha watu huku watu wote kutoka mji wa Fort McMurray wakiamrishwa kuondoka kutokana na moto.
Shughli za kuhamisha watu kwa lazima zinaendelea na zitaathiri karibu watu 80,000.
Mkuu wa mkoa ameiomba serikali kuu msaada wa kuwasafirisha watu kwa njia ya ndege.
Moto huo unaripotiwa kufunga barabara kuu inayotoka mjini humo.

4. Mkuu wa sheria Brazil amlaumu Lula

SilvaImage copyrightAP
Image captionLula da Silva anakabiliwa na tuhuma za ulaji rushwa
Mkuu wa sheria nchini Brazil amemlaumu rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva kwa kuhusika pakubwa kwenye sakata kubwa ya ufisadi inayoikumba kampuni ya mafuta ya serikali Petrobras.
Rodrigo Janot amesema kuwa ufisadi ambao unakisiwa kuigharimu kampuni hiyo karibu dola billioni mbili haungetokea bila ya Lula da Silva kushiriki.
Bw Janot ameiamia mahakama kuu kuamrisha uchunguzi kufanyika dhidi yake na wanasiasa wengine 29 maarufu, wafanyikazi wa umma na wafanyibiashara.
Rais huyo wa zamani amekana madai dhdi yake.

5. Kerry amuonya Assad kuhusu vita Aleppo

SyriaImage copyrightReuters
Image captionMapigano yanaendelea mjini Aleppo
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani amemuonya rais wa Syria Bashar al Assad kuwa kutakuwa na athari ikiwa serikali yake itakiuka usitishwaji wa mapigano mjini Aleppo unaojadiliwa kati ya Marekani na Urusi.
Bw Kerry amesema kuwa kukosa kuheshimu makubaliano hayo kutasababisha kurejea kwa vita kote nchini humo. Awali waziri wa mashauri ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov amesme kuwa usitishwaji ghasia mjini Allepo utatangawa muda mfupi ujao.

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © FURAHA MEDIA - Blogger Templates - Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -